Hili ni swali zuri sana ambalo kila mmoja anapaswa kujiuliza. Biblia inaongelea njia kuu mbili tu; njia ya kwenda Mbinguni na njia ya kwenda Jehanamu. Mbinguni ni sehemu yenye kila kitu kizuri, na ni makao ya Mungu. Jehanamu ni mahali pa dhambi na maharibifu yasiyo na mwisho. Ni sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya Shetani na watoto wake. Je,nifanye nini ili niweze kufika mahali ambapo ni nyumbani mwa Mungu? Kama wewe si mkristo sahihi, na haujazaliwa kwa mara ya pili, basi unahitaji wokovu.
27 Machi 2019 in Wokovu 6 minutes
Biblia hutuambia kwamba Mungu anajua kila kitu, na kwamba anahifadhi maandishi ya maisha yetu. Tutahitajika kutoa maelezo ya aliyoandika siku ya hukumu (Warumi 14:11-12). “Na niliwaona wafu, wadogo kwa wakubwa wamesimama mbele ya Mungu; na vitabu vilifunguliwa: na kitabu kingine cha uzima kikafunguliwa, na wafu walihukumiwa kwa yale yaliyoandikwa katika vitabu kulingana na kazi zao” (Ufunuo 20:12). Tutakaposimama katika hukumu mbele ya Mungu, tutakuwa tumechelewa kubadili maisha yetu wala mwisho wetu wa milele. CHAGUO NI LETU JE, JINA LAKO LIPO KATIKA KITABU CHA UZIMA? KUWA TAYARI KWA SIKU YA HUKUMU
22 Machi 2019 in Wokovu 4 minutes
Yesu anatuambia kwamba milango ya mbinguni imefungwa dhidi yetu isipokuwa tunazaliwa mara ya pili. Kwa hiyo twauliza: “Rafiki, umezaliwa mara ya pili?” “Muumini wa kanisa, umezaliwa mara ya pili?” Ikiwa hapana, basi umepotea. Kwa maana Yesu anasema, “Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu” (Yohana 3:3). Kwa kweli hakuna mtu anayetaka kufa akiwa mwenye dhambi, au kupotea; basi hamna budi kuzaliwa mara ya pili.
22 Machi 2019 in Wokovu 4 minutes
Kutambua Mbinu za Shetani kwa Kutumia Mwanga wa Neno la Mungu. Lengo la Biblia Takatifu silo kuangalia hasa Shetani na kazi zake. Japokuwa tunapata mengi kwenye Biblia yanayofunua tabia zake na kazi zake. Wakati fulani Shetani alikuwa malaika, lakini aligeuka kinyume cha Mungu, Muumba wake, na akatamani kuwa kama Mungu. Matendo ya ufalme wa giza wa Shetani siyo mageni. Yanaonyesha dhahiri jitihada za Shetani kwa miaka kupingana na Ufalme wa Mungu. Anatoa mbadala wa kile ambacho Mungu anatimiliza kwa kupitia nguvu za Roho Mtakatifu. Masomo Mengine: Luka 11:20-23 Mmoja mwenye nguvu zaidi ya Shetani Isaya 61:1 Kuwekwa huru mateka
22 Machi 2019 in Wokovu 6 minutes