Nyumbani

Karibu kwenye tovuti ya Gospel Tract and Bible Society

Trakti

Yesu anatuambia kwamba milango ya mbinguni imefungwa dhidi yetu isipokuwa tunazaliwa mara ya pili. Kwa hiyo twauliza: “Rafiki, umezaliwa mara ya pili?” “Muumini wa kanisa, umezaliwa mara ya pili?” Ikiwa hapana, basi umepotea. Kwa maana Yesu anasema, “Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu” (Yohana 3:3). Kwa kweli hakuna mtu anayetaka kufa akiwa mwenye dhambi, au kupotea; basi hamna budi kuzaliwa mara ya pili.

Wokovu 4 minutes

Tukabili hali halisi. Maovu ya kutisha - pombe, madawa ya kulevya, na zinaa - vinatishia na kuharibu kile kilichoubwa na Mungu kuwa kizuri. Vinakamata na kuwavuta wadogo kwa wakubwa kama mikono ya pweza mkubwa inavyoshika. Maambukizo kwa jamii ya leo ni makadirio makubwa. Watu wengi wamelegea bila nanga na kuachwa na laana ya pombe, madawa ya kulevya, na zinaa, wakielekea maangamizi ya milele. Watu wanavutwa upesi na wenzao, pamoja na matangazo yanayotolewa na video, radio, na magazeti kuhusu maovu hayo. Akili inashambuliwa mpaka inachanganyakiwa na kukaa na mawazo ya machafuko ambayo matokeo yake ni uharibifu wa kiroho na kimwili.

Maadili 4 minutes

Hili ni swali zuri sana ambalo kila mmoja anapaswa kujiuliza. Biblia inaongelea njia kuu mbili tu; njia ya kwenda Mbinguni na njia ya kwenda Jehanamu. Mbinguni ni sehemu yenye kila kitu kizuri, na ni makao ya Mungu. Jehanamu ni mahali pa dhambi na maharibifu yasiyo na mwisho. Ni sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya Shetani na watoto wake. Je,nifanye nini ili niweze kufika mahali ambapo ni nyumbani mwa Mungu? Kama wewe si mkristo sahihi, na haujazaliwa kwa mara ya pili, basi unahitaji wokovu.

Wokovu 6 minutes

“Tazama wapendezwa na kweli iliyo moyoni” (Zaburi 51:6). Uaminifu ni maadili ya ukweli katika kufungamana na mambo yote ya maisha. Kwa hakika uaminifu ni jambo la moyoni, pia ni fundisho la msingi la Injili ya Yesu Kristo. Mungu anajua mawazo na makusudi ya moyo. Anatambua ukweli kama msingi muhimu kwa maana yeye ni Mungu wa ukweli. (Kumb. 32:4) Hakika atabariki uaminifu uliokamilika wa moyo wetu. Je, unao tabia ya kusema ukweli wakati ungeweza kupatikana na jambo, lakini ukawa si mwaminifu wakati ambao hakuna atakayekugundua? Je, kwa makusudi unaweza kumridhisha mtu kwa ushawishi usio wa kweli?

Maadili 4 minutes

Je, wajua kwamba kuna mtu ambaye hujua yote juu yako? Ni Mungu aliyeumba ulimwengu na vitu vyote vilivyomo. Yesu, Mwana wa Mungu, pia hujua yote ambayo umeshafanya. Yeye hujua yaliyopita, ya leo, na yajayo. Yeye anakupenda na alikuja ulimwenguni kukuokoa kutoka dhambini. Anao mpango wa uzima wako ili kukuletea furaha. Siku moja Yesu alikuwa akitembea na rafiki zake alienda katika kijiji cha Samaria. Yesu alikaa kando ya kisima wakati rafiki zake walienda kununua chakula. Yesu alipokuwa amekaa pale, mwanamke mmoja alikuja kuchota maji kisimani. Yesu alimwambia, “Naomba unipe maji ninywe.”

Yesu, Upendo, Injili 3 minutes

Biblia hutuambia kwamba Mungu anajua kila kitu, na kwamba anahifadhi maandishi ya maisha yetu. Tutahitajika kutoa maelezo ya aliyoandika siku ya hukumu (Warumi 14:11-12). “Na niliwaona wafu, wadogo kwa wakubwa wamesimama mbele ya Mungu; na vitabu vilifunguliwa: na kitabu kingine cha uzima kikafunguliwa, na wafu walihukumiwa kwa yale yaliyoandikwa katika vitabu kulingana na kazi zao” (Ufunuo 20:12). Tutakaposimama katika hukumu mbele ya Mungu, tutakuwa tumechelewa kubadili maisha yetu wala mwisho wetu wa milele.

Wokovu 4 minutes

Je, wewe ni mwenye furaha? Au hofu na hatia huondoa furaha yako yote? Je, ungetamani kuondoa hatia yako, lakini hujui kwa njia gani? Huenda unajiuliza, “Je, nitawahi kuwa mwenye furaha tena?” Ninayo habari njema kwa ajili yako. Kuna Mmoja awezaye kukusaidia, kusamehe dhambi zako, na kukupa furaha ya daima. Jina lake ni Yesu. Ngoja nikuambie habari zake. Mungu ndiye mwenyewe aliyeumba ulimwengu na vitu vyote vilivyomo. Alikuumba wewe na mimi.

Yesu 3 minutes

Lengo la Biblia Takatifu silo kuangalia hasa Shetani na kazi zake. Japokuwa tunapata mengi kwenye Biblia yanayofunua tabia zake na kazi zake. Wakati fulani Shetani alikuwa malaika, lakini aligeuka kinyume cha Mungu, Muumba wake, na akatamani kuwa kama Mungu. Matendo ya ufalme wa giza wa Shetani siyo mageni. Yanaonyesha dhahiri jitihada za Shetani kwa miaka kupingana na Ufalme wa Mungu. Anatoa mbadala wa kile ambacho Mungu anatimiliza kwa kupitia nguvu za Roho Mtakatifu.

Wokovu 6 minutes

Yesu Rafiki Yako Ninaye rafiki. Yeye ndiye rafiki bora ambaye nimewahi kujua. Yeye ni mwema sana na mkweli ambaye na wewe pia ningependa umfahamu. Jina lake ni Yesu. Cha kustajaabisha ni kwamba na yeye angependa awe rafiki yako. Ngoja nikuambie habari zake. Tunasoma hadithi hii katika Biblia. Biblia ni kweli. Ni neno la Mungu. Mungu ndiye aliyeumba ulimwengu na vitu vyote vilivyomo. Yeye ni Bwana wa Mbinguni na dunia. Anatoa uzima na pumzi kwa viumbe vyote.

Yesu, Upendo, Urafiki, Upweke 2 minutes

Tunaishi katika ulimwengu ambamo kila mmoja hupenda kutoa udhuru. Karibu kwa kila jambo linalogusa moyo wako hutaki kukubali au kuukabili ukweli jinsi ulivyo, kwa hiyo unatafuta njia ya kujitetea, ukidhania kwamba utetezi wako utakuweka huru. Je, unafikiri udhuru zako zitakuweka huru mbele za Mungu? Je, kuokolewa kunao udhuru? Visingizio ulivyo navyo kwa uhakika havitakuweka huru. Adamu na Hawa walipotenda dhambi, kila mmoja alijaribu kumwekea mwenzake lawama ya dhambi iliyotendeka, wakidhania kwamba Mungu angeachilia dhambi yao kwani wametoa sababu ni kwa nini waliingia dhambini. Lakini bado twasoma katika Biblia kwamba Mungu aliendelea kuwaadhibu tu. Mungu hazikubali udhuru zetu, hata zipangiwe kwa hila ya namna gani, au hata ukijifanya uonekane kuwa msafi kiasi gani. (Mwanzo 3:9-19; Wagalatia 6:7-8).

Maisha Ya Mkristo 6 minutes

Bwana Yesu alikuja ulimwenguni kuwaokoa wanadamu kutoka kwa dhambi zao. “Bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa akawa ana mfano wa wanadamu” (Wafilipi 2:7). Alikufa kwa ajili ya dhambi za watu wote ulimwenguni, alizikwa na akafufuka tena (1Wakorintho 15:4), kisha akapaa kwenda mbinguni tena (Matendo 1:9). Mitume walimwona na pia waumini zaidi ya mia tano, baada ya kufufuka. Baada ya kupaa kwenda mbinguni, malaika wawili waliwaambia mitume kwamba kurudi kwake kutafanana na kupaa kwake. Ni Mungu tu ndiye anayefahamu ni lini Bwana atarudi. Huenda itakuwa ni jioni au usiku wa manane, au wakati wa asubuhi au alasiri. (Marko 13:35) “Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja” (Mathayo 24:44).

Maisha Yajayo 3 minutes