Baadhi wametabiri wakati wa kurudi kwake, hadi siku na saa. “Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila baba peke yake” (Mathayo 24:36). Atakuja haraka kama vile umeme utokavyo mashariki hadi magharibi (Mathayo 24:27). Atakuja wakati tusiotarajia kama mwizi anavyokuja usiku (2Petro 3:10). Siku hio itawajia kwa ghafla, kama mtego unasavyo (Luka 21:34). Bwana, katika hekima isiyo na vikomo, atarudi kumlipa kila mtu sawasawa na alivyotenda (Ufunuo 22:12). “Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, kesheni” (Marko 13:37). Dalili za Nyakati na za Kurudi Kwake
22 Machi 2019 in Maisha Yajayo 3 minutes