Je, wajua kwamba kuna mtu ambaye hujua yote juu yako? Ni Mungu aliyeumba ulimwengu na vitu vyote vilivyomo. Yesu, Mwana wa Mungu, pia hujua yote ambayo umeshafanya. Yeye hujua yaliyopita, ya leo, na yajayo. Yeye anakupenda na alikuja ulimwenguni kukuokoa kutoka dhambini. Anao mpango wa uzima wako ili kukuletea furaha. Siku moja Yesu alikuwa akitembea na rafiki zake alienda katika kijiji cha Samaria. Yesu alikaa kando ya kisima wakati rafiki zake walienda kununua chakula. Yesu alipokuwa amekaa pale, mwanamke mmoja alikuja kuchota maji kisimani. Yesu alimwambia, “Naomba unipe maji ninywe.”