Upendo

Siku moja Yesu alikuwa akitembea na rafiki zake alienda katika kijiji cha Samaria. Yesu alikaa kando ya kisima wakati rafiki zake walienda kununua chakula. Yesu alipokuwa amekaa pale, mwanamke mmoja alikuja kuchota maji kisimani. Yesu alimwambia, “Naomba unipe maji ninywe.” Mwanamke alishangaa, akasema, “Je, unaniomba maji unywe? Je, kwani hujui mimi ni Msamaria, na ninyi Wayahudi hamna uhusiano nasi?” Kwa upole Yesu alijibu, “Kama kwa hakika ungemjua Mungu, na ni nani anayeongea nawe, ungeniomba Mimi nikupe maji ya uzima, na ningeshafanya kwa furaha.” Mwanamke huyo alisema, “Bwana, nipe maji hayo ili nisipate kiu tena, wala nisihitaji kurudi kuchota maji hapa.”

Arabic Bengali Chinese Dutch English French German Haitian Creole Hindi Indonesian Italian Japanese Kazakh Khmer Kinyarwanda Korean Lingala Mossi Nepali (Macrolanguage) Norwegian Persian Plautdietsch Portuguese Punjabi Rundi Russian Southern Sotho Spanish Swedish Tajik Telugu Thai Turkish

22 Machi 2019 in  Yesu, Upendo, Injili 3 minutes

Yesu Rafiki Yako Ninaye rafiki. Yeye ndiye rafiki bora ambaye nimewahi kujua. Yeye ni mwema sana na mkweli ambaye na wewe pia ningependa umfahamu. Jina lake ni Yesu. Cha kustajaabisha ni kwamba na yeye angependa awe rafiki yako. Ngoja nikuambie habari zake. Tunasoma hadithi hii katika Biblia. Biblia ni kweli. Ni neno la Mungu. Mungu ndiye aliyeumba ulimwengu na vitu vyote vilivyomo. Yeye ni Bwana wa Mbinguni na dunia. Anatoa uzima na pumzi kwa viumbe vyote. Yesu alikuja duniani kama mtoto mchanga. Baba na Mama yake wa hapa duniani walikuwa Yosefu na Maria. Alizaliwa katika zizi na kulazwa horini.

Amharic Arabic Bemba (Zambia) Bengali Chinese Dutch English French German Haitian Creole Hindi Indonesian Japanese Kazakh Khmer Kinyarwanda Korean Lingala Malagasy Mossi Nepali (Macrolanguage) Norwegian Nyanja Oromo Persian Plautdietsch Polish Portuguese Punjabi Rundi Russian Southern Sotho Spanish Swedish Tajik Telugu Thai Tonga (Zambia) Turkish Ukrainian Uzbek Vietnamese

22 Machi 2019 in  Yesu, Upendo, Urafiki, Upweke 2 minutes