Tukabili hali halisi. Maovu ya kutisha - pombe, madawa ya kulevya, na zinaa - vinatishia na kuharibu kile kilichoubwa na Mungu kuwa kizuri. Vinakamata na kuwavuta wadogo kwa wakubwa kama mikono ya pweza mkubwa inavyoshika.
Maambukizo kwa jamii ya leo ni makadirio makubwa. Watu wengi wamelegea bila nanga na kuachwa na laana ya pombe, madawa ya kulevya, na zinaa, wakielekea maangamizi ya milele. Watu wanavutwa upesi na wenzao, pamoja na matangazo yanayotolewa na video, radio, na magazeti kuhusu maovu hayo. Akili inashambuliwa mpaka inachanganyakiwa na kukaa na mawazo ya machafuko ambayo matokeo yake ni uharibifu wa kiroho na kimwili.
Je, akina nani walaumiwe kwa nidhamu na mwenendo wa kuaibisha wa namna hii? Je, ni vijana? Siyo lazima. Kwa kutokumcha Mungu, maisha ya wazazi yamewaidhinishia dhambi ambazo kizazi cha vijana kinapenda. Akina baba na mama hawajui kwamba wanawafundisha watoto wao tabia mbaya ya madawa na ulevi kwa kushindwa kujizuia wenyewe. Kanuni za maadili ya Mungu zimeachwa kwa kutokujali. Kilio cha nguvu kingepanda juu mbinguni. Je, jinsi gani tujiokoe sisi na watoto wetu?
Miji yetu, shule zetu, na vyuo vyetu haziwezi kuzalisha raia katika kiwango kinachofaa kwa mataifa yetu ikiwa matumizi ya dawa za kulevya na pombe huvumiliwa na kuhimizwa kwa uzembe wa wazazi na waalimu.
Matumizi ya pombe ni uharibifu mkubwa wa maadili ya taifa, yakiharibu maamuzi, sifa, na maisha kwa ujumla. Huchangia kuvunjika na kugawanyika kwa familia, ambayo ni mojawapo baraka za Mungu kwa ajili ya wanadamu.
Zaidi, kuna ongezeko la matumizi ya madawa haramu. Madhara mabaya ya madawa haya ya kulevya ni makubwa zaidi ya faida yao.Utumiaji wa madawa ya kulevya inaweza kusababisha uharibifu wa akili. Watumiaji wa dawa za kulevya wanakubali kwamba hio ni mtego wa mauti: kiakili, kimwili, na kiroho. Uharibifu wa ubongo usiotibika, mauaji, na kujiua ni matokeo mabaya ya anasa hizi.
Kwa sababu ya tabia zao za asili kwa kutamani dhambi, watu wako tayari kufuata mwelekeo na tamaa zinazobuniwa na Shetani. Katika hali hii mwili unataka kuridhishwa pasipo kuzuiliwa. Zinaa hauzimi moto wa tama, bali inachochea. Kuzini siyo uponyaji kwa tamaa, kama vile pombe siyo tiba ya ulevi. Ukweli ni kwamba, tunapaswa kukabili tamaa zetu. Tamaa zinatokea miili yetu ambao itaishia hapa hapa duniani tutakapokufa. Nafsi zetu, yenye kudumu milele, inatamani kuheshimu amri za Mungu.
Uzinzi, Uasherati, Ushoga, Usagaji, na kujamiana na wanyama kumekatazwa na Neno la Mungu. (Walawi 18:23; Wagalatia 5:19-21). Uzinzi huleta maumivu, huzuni, maangamizi, hatia, na magonjwa ya zinaa. Usafi huleta busara ya kujistahifu na heshima. Tusidhani kwamba mtu anayetimiza tamaa zake ndiye mwenye uhuru wala mwenye furaha---hii ni uongo mkubwa. Atendaye dhambi ndiye mtumwa wa dhambi. Mwenye uhuru ndiye anayejikana na kutii sheria ya Mungu.
Wakati watu wametumbukia katika ziwa hilo la tope la ufisadi na upofu wa kiroho, na kuwa na ujasiri wa kutomcha Mungu, Biblia Takatifu imekwisha kujenga msingi ya nidhamu na haki. Bila shaka Biblia ndiyo yenye mamlaka ya milele juu ya masuala ya mema na mabaya. Mungu alimuumba binadamu na haja ya ngono kwa uzazi wa mataifa na kuimarisha au kuboresha kifungo cha ndoa kati ya mume na mke. Aliidhinisha kutimiza haja hii ndani ya ndoa iliyo halali tu. Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu. (Waebrania 13:4).
Mtume Paulo anaandika katika kitabu cha Warumi kuhusu hukumu ya Mungu juu ya kujamiana kijinsia moja (Ushoga/Usagaji). Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao. Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa, ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti; wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao. (Warumi 1:26-28,32). Hii ilikuwa ni dhambi ya Sodoma na Gomora iliyochukiza, na Mungu aliwaletea hukumu. (Mwanzo 19). Kulingana na maandiko ni haiwezekani kuwa na Roho Mtakatifu mioyoni mwetu wala kuishi maisha ya Mkristo ikiwa twafanya dhambi hizi.
Msomaji mpendwa, ili uwe na furaha halisi katika maisha, ili uwe na amani na Mungu, unapaswa kuwa na uhusiano naye. Tambua kwamba wewe ni mwenye dhambi na uungame, na uamini kwamba Yesu alikufa msalabani akichukua lawama yako. Ushindi unakusubiri!
Unapomfungulia Mungu moyo wako na kuziungama dhambi zako, atakusamehe. Tukizungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote. (1 Johana 1:9)
Kwa hiari mkabidhi Yesu maisha yako yote kama Mwokozi wako, na ufuate Neno lake pamoja na Roho Mtakatifu kwa utiifu kweli kweli. Baraka zinazopatikana katika maisha yaliyobadilika ni fikira safi zinazoleta mabadiliko ya ajabu katika matendo yetu na kazi zetu. Kristo atakupa ushujaa kukabili matatizo ya maisha na atakupa nguvu kushindia majaribu ambayo yaweza kukushambulia. Njoo kwa Yesu sasa wakati akikuita. Mtafuteni Bwana madamu anapatikana, mwiteni madamu yu karibu. (Isaya 55.6)