Vipeperushi
Amani, amani iko wapi—kwa mataifa, nyumbani kwetu, na zaidi ya yote kwa mioyo yetu? Kilio hiki kikuu kimesikika kwa vizazi. Je, ni kilio cha moyo wako pia? Watu wamechoka na kuhangaika. Bila shaka kuna haja ya mwongozo na ushauri, usalama na kujiamini. Tunahitaji na kutaka akili yenye utulivu. Akili yenye utulivu—Ni hazina iliyoje! Je, hazina hii inaweza kupatikana katika ulimwengu wenye mizozo na kukata tamaa, wenye misukosuko na matata?
Yesu anasema kwamba milango ya mbinguni imefungwa dhidi yako isipokuwa unazaliwa mara ya pili. Kwa hiyo twauliza: “Rafiki, umezaliwa mara ya pili?” “Muumini wa kanisa, umezaliwa mara ya pili?” Ikiwa hapana, basi umepotea. Kwa maana Yesu anasema, “Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu” (Yohana 3:3). Kwa kweli hakuna mtu anayetaka kufa akiwa mwenye dhambi, au kupotea; basi hamna budi kuzaliwa mara ya pili.
Tukabili hali halisi. Maovu ya kutisha - pombe, madawa ya kulevya, na zinaa - vinatishia na kuharibu kile kilichoubwa na Mungu kuwa kizuri. Vinakamata na kuwavuta wadogo kwa wakubwa kama mikono ya pweza mkubwa inavyoshika. Maambukizo kwa jamii ya leo ni makadirio makubwa. Watu wengi wamelegea bila nanga na kuachwa na laana ya pombe, madawa ya kulevya, na zinaa, wakielekea maangamizi ya milele. Watu wanavutwa upesi na wenzao, pamoja na matangazo yanayotolewa na video, radio, na magazeti kuhusu maovu hayo. Akili inashambuliwa mpaka inachanganyakiwa na kukaa na mawazo ya machafuko ambayo matokeo yake ni uharibifu wa kiroho na kimwili.
Hili ni swali zuri sana ambalo kila mmoja anapaswa kujiuliza. Biblia inaongelea njia kuu mbili tu; njia ya kwenda Mbinguni na njia ya kwenda Jehanamu. Mbinguni ni sehemu yenye kila kitu kizuri, na ni makao ya Mungu. Jehanamu ni mahali pa dhambi na maharibifu yasiyo na mwisho. Ni sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya Shetani na watoto wake. Je,nifanye nini ili niweze kufika mahali ambapo ni nyumbani mwa Mungu? Kama wewe si mkristo sahihi, na haujazaliwa kwa mara ya pili, basi unahitaji wokovu.
“Tazama wapendezwa na kweli iliyo moyoni” (Zaburi 51:6). Uaminifu ni adili la ukweli linalofungamana na mambo yote ya maisha. Kwa hakika uaminifu ni jambo la moyoni, pia ni fundisho la msingi la Injili ya Yesu Kristo. Mungu anajua mawazo na makusudi ya moyo. Anatambua ukweli kama msingi muhimu kwa maana yeye ni Mungu wa ukweli. (Kumb. 32:4) Hakika atabariki uaminifu uliokamilika wa mioyo yetu. Je, unayo tabia ya kusema ukweli wakati mambo yako yangedhihirika, lakini ukawa si mwaminifu wakati ambao hakuna atakayekugundua? Je, kwa makusudi ungeweza kumridhisha mtu kwa ushawishi usio wa kweli?
Je, wajua kwamba kuna mtu ambaye hujua yote juu yako? Ni Mungu aliyeumba ulimwengu na vitu vyote vilivyomo. Yesu, Mwana wa Mungu, pia hujua yote ambayo umeshafanya. Yeye hujua yaliyopita, ya leo, na yajayo. Yeye anakupenda na alikuja ulimwenguni kukuokoa kutoka dhambini. Anao mpango wa uzima wako ili kukuletea furaha. Siku moja Yesu alikuwa akitembea na rafiki zake alifikia kijiji cha Samaria. Yesu alikaa kando ya kisima wakati rafiki zake walienda kununua chakula. Yesu alipokuwa amekaa pale, mwanamke mmoja alikuja kuteka maji kisimani. Yesu alimwambia, “Naomba unipe maji ninywe.”
Je, wajua kwamba kuna kitabu ambacho hueleza jinsi dunia ilivyoanzishwa? Maneno ya kwanza ya kitabu hiki ndiyo, “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi”. Kufuata maneno haya inaeleza jinsi dunia ilivyoumbwa na kuhusu mwanamume wa kwanza na mwanamke walioishi duniani. Inatuambia si tu kuhusu mwanzo wa muda, lakini pia ni kile kitakachotokea maisha haya yakiisha. Katika kitabu hiki chote, twasoma jinsi tunavyopaswa kuishi ili tuandaliwe kwa maisha baada ya kifo.
Hofu ni nini? Hofu ya Mungu Hofu ya wakati ujao Hofu ya kushindwa Hofu ya mateso Hofu ya kifo Hofu, adui wa siri, huvamia watu wa kila umri na utaifa, na kila hatua ya maisha. Ni hila na ya kuumiza, hutia sumu namna yetu ya kufikiri, huiba furaha yetu ya ndani, na huua hamu yetu ya kuishi. Inatufanya tuwe na wasiwasi, wanyonge, wenye mshituko, wenye mahangaiko, kukasirika na wenye moyo dhaifu: Ni hisia gani hizi mbaya sizizohitajika!
Maisha ni magumu. Mateso na magumu ni sehemu ya maisha yetu. Watu wengi kwa wakati mwingine wanaugulia magonjwa ya kimwili. Njaa inawashikia watu kwa asilimia kubwa hapa duniani. Umasikini unawatesa watu wasio na uwezo. Na wengine wapo wanaoteseka mikononi mwa watu kwa namna mbalimbali. Kwa mfano, baadhi wanashikwa na matatizo ya kindoa, au wazazi wakatili, au mabwana wakali. Kwa sababu ya hali ya vita katika baadhi ya nchi zingine watu wengi wasio na hatia wanapoteza mali, nyumba, familia, na hata maisha yao. Wale wanaomtumikia Mungu kwa uaminifu, wanateswa na kuudhiwa kwa sababu ya imani yao. Ulimwenguni pote watu mamilioni wanateseka kila siku. Kwa nini?
Biblia hutuambia kwamba Mungu anajua kila kitu, na kwamba anahifadhi maandishi ya kumbukumbu za maisha yetu. Tutahitajika kutoa maelezo ya aliyoandika siku ya hukumu (Warumi 14:11-12). “Na niliwaona wafu, wadogo kwa wakubwa wamesimama mbele ya Mungu; na vitabu vilifunguliwa: na kitabu kingine cha uzima kikafunguliwa, na wafu walihukumiwa kwa yale yaliyoandikwa katika vitabu kulingana na kazi zao” (Ufunuo 20:12). Tutakaposimama katika hukumu mbele ya Mungu, tutakuwa tumechelewa kubadilisha maisha yetu wala mwisho wetu wa milele.