Baadaye

Hapo mwanzo, Mungu aliumba mbingu na nchi. Aliumba jua, mwezi, na nyota, na pia mimea na wanyama. Siku ya sita, aliumba mtu kwa mfano wake na akampulizia puani pumzi ya uhai. Mtu huyu wa kwanza alikuwa Adamu, na jina la mkewe aliitwa Eva. Mungu aliwapa makao ya kuishi katika bustani nzuri ya Edeni. Mungu aliwapenda Adamu na Eva, nao walimpenda Mungu. Mungu alimwagiza Adamu kuitunza bustani. Mungu aliwaambia kua wanaweza kula chochote watakacho isipokuwa kwa mti wa ujuzi wa mema na mabaya, na ya kuwa watakufa kama hawatatii.

Baadaye, Injili, Mbinguni, Color 3 minutes

Imeandikwa na John Reynolds Mojawapo ya mifano iliyohai na ya kuvutia kabisa ya kurudishiwa uhai wa mtu aliyekwisha kufa ambao nimewahi kuufahamu ulikuwa ni ule wa George Lennox, mwizi stadi wa farasi kutoka Jimbo la Jefferson (Marekani). Alikuwa akitumikia kifungo chake cha pili. Jimbo la Sedwick lilimpeleka gerezani kwa mara ya kwanza kwa kosa hilo hilo – wizi wa farasi.

Baadaye 11 minutes

Je, ni kwa “njia ya Yesu Kristo”? Au ni kwa “njia ya kimwili”? Njia ya Yesu Kristo ni njia nyembamba. Inaongoza kwenda Mbinguni. Huko Mbinguni hakutakuwa na huzuni wala maumivu, bali furaha na faraja pamoja na Yesu na malaika watakatifu. Njia ya kimwili ni njia pana. Inatuelekeza kwenye maangamizi, yaani Jehanamu, mahali ambapo kutakuwa na maumivu, maombolezo, na kusaga meno. Ili kuenenda katika njia ya Yesu Kristo, lazima tuachane na njia ya kimwili. Yesu alisema, “Mtu yeyote akitaka kuwa mfuasi wangu, lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate.” (Mathayo 16:24). Je, kujikana nafsi kunamaanisha nini?

Baadaye, Africa 4 minutes