Hakuna utafutaji uliofanyika
Hakuna utafutaji wa hivi majuzi
Hakuna matokeo kwa "Query here"
Tafuta kwa FlexSearch
Ukurasa unaotafuta haupo au umehamishwa.
Mwanamume mmoja kijana alifiwa mke wake wakati mtoto wake wa kiume akiwa bado mdogo. Kwa maangalizi ya makini na ya woga kabisa huyo baba aliweza kumlea yule mtoto. Kwa kuwa kijana alikuwa ni mboni ya jicho lake, alimpa vitu vingi, na alimpa chakula bora kabisa kilichokuwa kinapatikana. Baada tu ya yule mwanaume kupona na mawazo ya kumpoteza mke wake mpendwa, mtoto wake wa kiume aliugua na alikuwa na hali mbaya sana. Daktari aliagiza dawa ya kuponya ugonjwa wake. Dawa ile ilikuwa na ladha ya uchungu, kwa hiyo yule kijana hakutaka kuinywa. Kila mara baba yake alikuwa anamlazimisha kunywa ile dawa.
Kila mahali watu wote hutamani kuwa na vitu vya kupendeza kwa maisha yao. Kila mmoja angependa kuwa na chakula kizuri, na cha kutosha kugawanya kwa marafiki na wageni; nguo zilizokamilika, na za kutosha kubadili kwa wakati mbalimbali; nyumba nzuri, imara na kubwa ya kutosha, yenye paa nzuri kwa majira yote. Pia tunatarajia kuwa na kiasi cha fedha mkononi ili kukabili matumizi yote, shughuli zetu, kwa dawa ukijitokeza ugonjwa, na hata ya kutosha kusafiria kuwaona marafiki mahali pengine. Kila mmoja hutaka dhamana ya kufanikiwa, hata kuwa na pesa za ziada mkononi kumaliza shida za dhorura.
Je, ni kwa “njia ya Yesu Kristo”? Au ni kwa “njia ya kimwili”? Njia ya Yesu Kristo ni njia nyembamba. Inaongoza kwenda Mbinguni. Huko Mbinguni hakutakuwa na huzuni wala maumivu, bali furaha na faraja pamoja na Yesu na malaika watakatifu. Njia ya kimwili ni njia pana. Inatuelekeza kwenye maangamizi, yaani Jehanamu, mahali ambapo kutakuwa na maumivu, maombolezo, na kusaga meno. Ili kuenenda katika njia ya Yesu Kristo, lazima tuachane na njia ya kimwili. Yesu alisema, “Mtu yeyote akitaka kuwa mfuasi wangu, lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate.” (Mathayo 16:24). Je, kujikana nafsi kunamaanisha nini?