Hofu ni nini?
Hofu ya Mungu
Hofu ya wakati ujao
Hofu ya kushindwa
Hofu ya mateso
Hofu ya kifo
Hofu ni nini
Hofu, adui wa siri, huvamia watu wa kila umri na utaifa, na kila hatua ya maisha. Ni hila na ya kuumiza, hutia sumu namna yetu ya kufikiri, huiba furaha yetu ya ndani, na huua hamu yetu ya kuishi. Inatufanya tuwe na wasiwasi, wanyonge, wenye mshituko, wenye mahangaiko, kukasirika na wenye moyo dhaifu: Ni hisia gani hizi mbaya sizizohitajika!
Tunahofia migogoro na mabadiliko, kushindwa na kuchanganyikiwa. Baadhi ya watu wanahofia ugonjwa na mateso. Wengine wana hofu mabaya kuwapata wapendwa wao. Wengine huhofia watu wengine na maoni yao. Wengine wanahofia giza, au kua peke yao. Wengi huogopa kufa na kukabiliana na yasiyojulikana. Kuna wakristo wanaohofu ya kua wokovu wao hauko salama, au kua Mungu hajawasamehe dhambi zao. Hawaogopi tu kufa, ila pia wanaogopa kuishi.
Hofu huingia polepole na kwa kimya katika fikra zetu hivyo ni kazi kutambua kua tunakua wahanga wa ushawishi wake wa uharibifu. Hata hofu kidogo tu kama tone la rangi katika glasi ya maji hubadili rangi ya kila kitu. Iwapo mkondo huu mwembamba wa hofu hautazuiwa , unakata mfereji ambao mawazo mengine huelekezwa.
Maisha ni tata, dunia ina vurugu, lakini matatizo ya nje hayapaswi kuvuruga amani ya ndani. Ni hofu ya ndani ambayo twapaswa kukabiliana nayo. Hofu huingia wakati mahitaji yetu muhimu zaidi yanaposhindwa kutimizwa. Roho zetu, zimefanywa kwa sura ya Mungu, mlilie yeye. Tunapokua mbali na Mungu tutarajie kujazwa na mashaka, utata, na hofu.
Shetani hutumia vema hofu zetu. Katika kila fursa huiongeza na kuifanya ionekane kua ni halisi na yenye mantiki. Njia yetu hua giza zaidi na zaidi , na mizigo iliyoko moyoni hua mizito zaidi na zaidi, hadi tupoteze matumaini yote ya ukombozi.
Shetani hufanya kazi gizani. Hawezi kufanya kazi katika nuru kwa sababu, “Mungu ni nuru, na katika yeye hakuna giza kabisa (1 Yohana 1:5). Shetani anajua udhaifu wetu, na katika maeneo hayo huleta mawazo na hofu. Hutafuta kuharibu ukweli na kutuchanganya kwa uongo. Kama tukiyaacha mambo haya yafunikwe na giza la mioyo yetu na mawazo yetu, shetani ataendeleza kazi kazi zake za uovu wa kutukatisha tamaa na hofu. Anaweza kushindwa na nguvu zake zinaweza kurudishwa nyuma kama tukimfunua kwenye nuru.
Hofu ya Mungu
Dhambi husababisha kulemewa na hofu inayotokana na maarifa kua maisha ya mtu hayampendezi Mungu. Ilikua siku ya huzuni pale Adamu na Eva walipovuna kutokana na mapendekezo kutoka kwa shetani kua wasitii amri ya Mungu ya kutokula katika mti ulio katikati ya bustani. Kutokana na kutotii walitenda dhambi na baadaye wakajificha mbali na uwepo wa Mungu. Jioni ile Mungu aliwaita, na Adamu akasema “Nalisikia sauti yako katika bustani nami nikaogopa” (Mwanzo 3:10). Katika vizazi tangu Adamu, watu wote wamepita chini ya kivuli hiki cha dhambi. Hofu hii ya hukumu ya Mungu, kama itamsogeza mtu kutubu dhambi zake, itakua nguvu chanya katika maisha ya mtu. “Kumcha Bwana ni mwanzo wa hekima” (Zaburi 111:10). Hii ndio heshima na hofu sahihi tunayohisi. Tunaona kwa sehemu ukuu wa Mungu, Haki yake, Hukumu zake,Upendo wake, huruma zake, Hekima zake,na umilele wake. Yeye ajuaye yote, Mwenye nguvu zote,na aliyepo milele. Tunatambua kua kuwepo kwetu kupo katika mikono yake na sisi ni kazi ya mikono yake.Tunaogopa kutompendeza Mungu wa namna hii. Tunajua kwamba haki ya Mungu hutoa hukumu ya jehanamu ya moto kwa wanaoishi katika dhambi “Maana kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa wa ile kweli , haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao” (Waebrania 10:26-27). Maarifa haya huleta hofu ya dhambi. Pale tunaanza kumjua Mungu kama rafiki yetu binafsi kupitia toba, msamaha na kutii, huduma yetu Kwake inahamasishwa na hofu ya Kimungu, na kwa upendo na shukurani na zawadi ya wokovu isiyotamkwa. “Katika pendo hamna hofu : lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu ; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo” ( 1 Yohana 4:18). Hofu yetu kwake si ile inayoamsha hofu katika mioyo yetu, lakini ile inayoongeza upendo wetu Kwake. Tutakapoitumia kwa uhakika katika maisha yetu, hii ni hofu pekee inayoweza kushinda hofu zingine zote. Kwa nini sasa wengi wanaruhusu wingu la hofu kukamata mioyo yao, kutaabisha mawazo yao, na kufunika njia ya maisha? Njia ya Mungu ni njia ya amani na kuaminika.
Kuna hadithi iliyosimuliwa ya mvulana mdogo aliyekua anaogopa kutembea mwenyewe usiku wa giza, lakini baba yake alipotembea karibu naye na kumshika mkono wake hofu yote ilitoweka. Giza sasa likawa haliogopeshi, kwa sababu alimpenda na kumwamini baba yake, na alijua ya kua atamtunza. Hapa kuna funguo ya sisi kua huru mbali na hofu: tunapaswa kujifunza kumjua Mungu wetu wa mbinguni vema. Tunapomjua Mungu, tunamtegemea Yeye kabisa katika maisha yetu, tunaweka mikono yetu salama katika mikono Yake. Tunaongea naye kwa unyenyekevu juu ya maswali yanayoumiza akili zetu, na huzuni za maisha ambazo zinaweza kutufanya tukate tamaa.
Tunao mfano wa mtume Petro, pale Yesu alimwambia atembee juu ya dhoruba ya mawimbi ya bahari ya galilaya. Petro hakuogopa hadi wakati alipoacha kumtazama Bwana, na kuanza kuangalia mawimbi yanayotisha. Hapo alianza kuzama, ( Mathayo 14: 24-31). Tunapotafuta uhuru kutoka kwenye hofu na kuweka tumaini kwa Mungu, Roho wake atazungumza na sisi kwa sauti yake ndogo ya upole. Tunapomtazama yeye badala ya hofu zetu, dhoruba hutulia. Yeye sasa hujibu maswali yanayotufadhaisha, hubadili mashaka yetu kwa uhakika, na kutushika mkono wetu kwa utulivu katika mkono wake. Tunaweza, kwa neema yake, kushinda madhara ya ulemavu wa hofu.
Hofu ya wakati ujao
Fumbo la mambo yajayo yasiyojulikana hufanya baadhi ya watu kuwa na wasiwasi. Kila asubuhi wanaamka katika siku isiyotabirika. Wanakabiliana na masumbuko “itakuwaje” wakati huo fikra zao zikikimbilia katika njia zenye giza la wasiwasi mkubwa wa kufikirika. “ msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu” (Wafilipi 4:6). Kwa kutumaini wakati ujao katika mikono ya Mungu, tunaachilia Kwake mizigo ya mambo yasiyojulikana. Jaribu hili na uone!
Wengi wanahofia yajayo kwa sababu wanakosa dira ya maisha yao. Kwa kutokujua mahali waendako, wanahisi mabaya. Mungu anajua yaliyopo mbele, na watakapomruhusu Yeye kuwaongoza, maisha yao yatakua si safari ya kutangatanga, bali njia ya kuelekea nyumbani.
Mungu ameahidi kuwa mwaminifu kwao wanaomuamini ijapokua wanakutana na wakati ujao usiojulikana. Unaamini hilo? Haijalishi dhoruba ni kali kiasi gani, au giza la usiku, au mlima mrefu, Atakupitisha.
Hofu ya kushindwa
Tuna shauku ya kufanikiwa, lakini tuna hofu kua tutashindwa wenyewe, familia zetu, na maisha yenyewe kama yalivyo. Tunahofu kua tutafanya chaguo lisilo sahihi na kufanya mpango usio sahihi.
Mungu alimuamuru Johua , “uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kua BWANA , Mungu wako , yu pamoja nawe kila uendako ( Yoshua 1:9). Tunapoweka maisha yetu chini ya usimamizi wa Bwana, kushindwa kwa mambo yaliyopita si mwisho; yanaweza kua daraja la mafanikio.
Hofu ya mateso
Sisi sote tunachoshwa na mawazo ya maumivu ya mwili, uchungu wa kukosolewa, maumivu ya ukiwa na huzuni. Mungu hatatufunika kutoka katika mateso yote, lakini atatupa neema ya kustahimili. Ameahidi amani na uhakika katikati ya mateso yetu. “ Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa” (Zaburi 46:1-2). Kama tunampenda Bwana , atatumia mateso kwa mema yetu. Mateso yanatoa nafasi ya kujua uwepo na viwango vya nguvu ya Mungu.Pia inaongeza kina cha tabia na moyo wa maarifa. Mateso yanaweza kututengeneza au kutubomoa.Je yatakuwaje kwako?(Which will it be?)
Hofu ya kifo
Hofu ya kifo ni ya kawaida sana kwa wanadamu. Kusema kwaheri ni jambo la kuumiza sana.
Tunapaswa kutia mkazo kwa swali hili la zamani, “ kama mtu akifa, je ataishi tena?”(Ayubu 14:14). Yesu alikuja kutukomboa kutoka katika hofu ya kifo. (Waebrania 2: 14-15). Ndiyo maana alikufa na akafufuka, na ndiyo maana alituahidi, “ Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakua hai” (Yohana 14:19). Katika yeye kifo sio mlango wa ubatili , bali lango ling’aalo kuingia maisha mapya. “msifadhaike mioyoni mwenu…… nyumbani mwa baba yangu mna makao mengi… maana naenda kuwaandalia mahali” (Yohana 14: 1-2). Itakua mahali palipoandaliwa kwa ajili ya watu waliojiandaa.
Je umejiandaa? Je umetubu kwa ajili ya maisha yako ya dhambi? Toba huondoa dhambi za nyuma na kugeuka kutoka katika maisha ya kale. Ni lini ilikua mara yako ya mwisho kwenda mbele za Mungu kwa maombi na kumpa mzigo wako wa kutunzwa, wasiwasi wako na hofu? Yesu anasema , “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha” (Mathayo 11:28). Ni Mwaliko wa namna gani! Ni Ahadi ya namna gani!
Njoo-ukiamini, ukiomba, ukiwa na matumaini, nawe utapata amani.
Njoo-nawe utajua furaha ya kuishi maisha yenye pumziko. Mungu anakualika kumuamini Yesu Kristo na uwe huru, huru mbali na hofu. Njoo!