Je, wajua kwamba kuna kitabu ambacho hueleza jinsi dunia ilivyoanzishwa? Maneno ya kwanza ya kitabu hiki ndiyo, “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi”. Kufuata maneno haya inaeleza jinsi dunia ilivyoumbwa na kuhusu mwanamume wa kwanza na mwanamke walioishi duniani. Inatuambia si tu kuhusu mwanzo wa muda, lakini pia ni kile kitakachotokea maisha haya yakiisha. Katika kitabu hiki chote, twasoma jinsi tunavyopaswa kuishi ili tuandaliwe kwa maisha baada ya kifo.
Kitabu hiki cha zamani sana kiliandikwa karibu na waandishi 40 tofauti katika kipindi cha takribani miaka 1500. Waliandika kile walichoambiwa kuandika. Mungu aliwaambia waandishi juu yake mwenyewe. Mwandishi wa kitabu cha Mwanzo, ndicho kitabu cha kwanza, aliandika juu ya uumbaji na pia kuhusu maji yaliyoifunika nchi. Yeye na wengine waliandika kuhusu watu waliochaguliwa na Mungu. Mungu aliwaongoza wanaume mbalimbali waandike historia, mashairi, unabii, na kuhusu ahadi za Mungu. Kwa sababu ya maandiko haya yaliongozwa na Mungu, hapana jina lolote la mtu kwenye kava yake. Inaitwa Biblia ambayo maana yake ni “kitabu.” Mara nyingi inaitwa Biblia Takatifu imaanishayo “kitabu kitakatifu.”
Biblia ni kitabu kinachozidi kusambazwa duniani kote. Ingawa kumekuwa na nyakati ambapo wengine wamejaribu kuiharibu, Mungu ameihifadhi sikuzote na ataihifadhi daima. “Bali Neno la Bwana hudumu hata milele.” (1Petro 1:25). Biblia inatokana na vitabu 66. Imegawanyika katika sehemu mbili — Agano la Kale na Agano Jipya. Agano la Kale huongelea historia ya ulimwengu na jinsi Mungu alivyoahidi kumtuma mwanawe Yesu duniani kutuokoa sisi kutoka dhambi zetu. Agano Jipya huongelea jinsi Yesu alivyozaliwa kama mtoto. Matokeo mengi ya maisha ya Yesu yameandikwa, kujumuisha miujiza mingi aliyoitenda. Biblia inatuonyesha kwamba Yesu ni mfano wetu mkamilifu katika mambo yote. Alipozungumza Yesu, watu waliyasikiliza mafundisho yake. Tunaweza kusoma mengi yao kwenye vitabu viitwavyo Injili.
Injili ya Yohana ina maneno mengi ya Yesu. Aliwaambia watu kwamba Mungu ndiye Baba yake. Alifundisha kwamba Mungu anapenda kila mmoja duniani. Yohana 3:16 husema “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Twasoma pia jinsi Yesu alivyoteseka na kufa ili azilipie dhambi zetu na kwamba alifufuka kutoka wafu kuishi milele. Yesu hutuambia kwamba tunaweza kupata msamaha wa dhambi zetu tukimwamini Yeye. Kwa sababu kitabu cha Yohana ina maneno mengi ya Yesu, nacho ni rahisi kueleweka, ni mojawapo ya vitabu vya kwanza vya Biblia ambavyo tunapaswa kusoma.
Je, umewahi kujiuliza ni nini kitatokea baada ya maisha kuisha? Biblia hutuambia kwamba siku moja Yesu atakuja tena kuhukumu watu wote. Tunaweza kusoma jinsi ya kujitayarisha kwa ajili ya wakati ule. Yesu hutuambia kwamba alienda kuandaa sehemu Mbinguni kwa ajili ya wale watakaomkubali.
Katika Biblia tunapata majibu ya maswali ya kutatanisha maishani. Tulitokea wapi? Kwa nini tupo hapa? Tukifa tataenda wapi? Maswali haya na mengine yanajibiwa katika Biblia yote. Maisha yanapokosa lengo, tunaweza kwenda kwenye Biblia ambapo Mungu asema, “Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama” (Zaburi 32:8). Akifa mtu aliye karibu kwetu, tunaweza kuiendea Biblia kupata faraja kwa Mungu. Anaitumia Biblia kuongea nasi leo.
Wakati mwengine twasoma kitabu na tunajiuliza ikiwa ni kweli. Tunajua Biblia ni kweli kwa sababu ndiyo Neno la Mungu. Kuna maelfu ya mistari katika Biblia yenye maneno haya, “Bwana asema hivi.” Kuna unabii mwingi ambao umeandikwa na baadaye ulitimizwa kama ulivyotabiriwa. Yesu aliahidi kutoa amani na furaha kwa waendao kwake. Wengi wameona hili. Kakita upendo wake Mungu kwa binadamu, ametolewa Neno lake kwa wote. Biblia huzungumzia mioyo yetu.