Hapo mwanzo, Mungu aliumba mbingu na nchi. Aliumba jua, mwezi, na nyota, na pia mimea na wanyama. Siku ya sita, aliumba mtu kwa mfano wake na akampulizia puani pumzi ya uhai.
Mtu huyu wa kwanza alikuwa Adamu, na jina la mkewe aliitwa Eva. Mungu aliwapa makao ya kuishi katika bustani nzuri ya Edeni. Mungu aliwapenda Adamu na Eva, nao walimpenda Mungu. Mungu alimwagiza Adamu kuitunza bustani. Mungu aliwaambia kua wanaweza kula chochote watakacho isipokuwa kwa mti wa ujuzi wa mema na mabaya, na ya kuwa watakufa kama hawatatii.
Siku moja jambo baya lilitokea! Adamu na Eva walitenda dhambi baada ya kutomtii Mungu na kula matunda ya mti uliokatazwa. Wakaanza kumwogopa Mungu na kujificha na Yeye.
Mungu alijua mahali walijificha. Alikuja na kumwita Adamu. Mungu akamwambia kwa sababu hawakutii , walitakiwa kuacha mji wao mzuri wa bustanini.
Mungu hakuwasahau Adamu na Eva. Aliendelea kuwapenda. Aliahidi kumtuma mwanawe wa pekee Yesu ulimwenguni. Yesu angefariki kwa ajili ya dhambi zao ili waweze kuishi! “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” (Yohana 3:16)
Yesu alikuja! Alifundisha ya kuwa watu wote wametenda dhambi. Wenye dhambi lazima wafe. Yesu alitupenda sana hata akamwambia Mungu kuwa atakufa kwa ajili ya dhambi za watu wote. Alikufa kwa ajili ya kila mtu aliyekosea.
Habari njema-Yesu yu hai. Alifufuka kutoka kaburini! Alisema,“Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima….” ( Yohana 14:6). Yesu anataka kutuongoza kwenye makao kwa Baba yake wa mbinguni.
Wakati mwingine hatujihisi kupendwa. Watu waliotuzunguka wana huzuni, wameumizwa, ama wana hasira. Pengine tunaogopa ama tuna shauku(hamu) ndani yetu isiyoisha. Tunajiuliza, nani atatusaidia, na kwa nini tunahisi upweke sana. Mungu aliweka hiyo shauku ndani ya mioyo yetu kwa sababu anatupenda. Ni jambo maalumu linalotusogeza kwa Baba yetu wa mbinguni. Mungu anataka kubadili hiyo shauku ndani ya mioyo yetu kwa upendo wake.
Anataka uombe kutoka ndani ya moyo wako na kusema, “Yesu, ninakuhitaji. Nimechoka na dhambi zangu. Tafadhali Yesu, nioshe niwe safi nami nitaacha haya mambo yote mabaya”. Yesu anasikia ombi la moyo wako. Anakusafisha uwe safi na kukufanya tayari kwa makao anayoandaa.
Kabla ya Yesu hajaondoka duniani, Alisema, “Msifadhaike mioyoni mwenu: mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.” (Yohana 14:1-2). Hayo makao ya Mbinguni ni mahali penye amani na kuna furaha na upendo usio na kikomo.
Yesu amefanya hayo makao kuwa mazuri sana na hataruhusu ubaya wowote ama dhambi ndani yake.
Ikiwa tutakufa na mioyo yetu ina madoa ya dhambi, Yesu hatatukaribisha.
Itakuwaje kuishi na Yesu? Hakutakuwa na maumivu tena, wasiwasi, ama njaa. Hakuna magonjwa tena, kifo, ama kuagana kwa huzuni. Huko tutaimba na kumsifu Mungu na wote waliokombolewa na dunia.
Hatimaye nyumbani! Nyumbani mbinguni pamoja na Yesu mwokozi wetu!