Yesu Rafiki Yako Ninaye rafiki. Yeye ndiye rafiki bora ambaye nimewahi kujua. Yeye ni mwema sana na mkweli ambaye na wewe pia ningependa umfahamu. Jina lake ni Yesu. Cha kustajaabisha ni kwamba na yeye angependa awe rafiki yako. Ngoja nikuambie habari zake. Tunasoma hadithi hii katika Biblia. Biblia ni kweli. Ni neno la Mungu. Mungu ndiye aliyeumba ulimwengu na vitu vyote vilivyomo. Yeye ni Bwana wa Mbinguni na dunia. Anatoa uzima na pumzi kwa viumbe vyote. Yesu alikuja duniani kama mtoto mchanga. Baba na Mama yake wa hapa duniani walikuwa Yosefu na Maria. Alizaliwa katika zizi na kulazwa horini.