Mwanamume mmoja kijana alifiwa mke wake wakati mtoto wake wa kiume akiwa bado mdogo. Kwa maangalizi ya makini na ya woga kabisa huyo baba aliweza kumlea yule mtoto. Kwa kuwa kijana alikuwa ni mboni ya jicho lake, alimpa vitu vingi, na alimpa chakula bora kabisa kilichokuwa kinapatikana.
Baada tu ya yule mwanaume kupona na mawazo ya kumpoteza mke wake mpendwa, mtoto wake wa kiume aliugua na alikuwa na hali mbaya sana. Daktari aliagiza dawa ya kuponya ugonjwa wake. Dawa ile ilikuwa na ladha ya uchungu, kwa hiyo yule kijana hakutaka kuinywa. Kila mara baba yake alikuwa anamlazimisha kunywa ile dawa.
Baada ya dozi yule kijana akasema, “Baba kwa nini unanilazimisha kunywa hii dawa mbaya hivi, kwa nini hukununua dawa yenye ladha nzuri?” Kwa machozi ya upendo baba akajibu, “Oh kijana wangu, hii ndiyo iliyoagizwa. Kama nisingekupa hii dawa ungeugua zaidi na kufariki. Nataka uishi maisha marefu zaidi ya mama yako.”Machozi zaidi yalitiririka kwenye mashavu yake na midomo yake ikashindwa kuongea zaidi. Alimchukua mtoto na kumweka alale kwenye mabega yake kwa moyo wa upendo.
“Baba,” alisema mtoto hatimaye, “dawa ni chungu, lakini nitaendelea kunywa kwa kuwa naelewa kila dozi itanisaidia niendelee kujisikia vizuri. Mimi ni kijana wako, nitafanya kama ulivyosema.”
Wanaume na Wanawake kila mahali, wakati majaribu, kushindwa, na bahati mbaya zinapokuja kwenye maisha yako, waza kama huyu kijana. Twaweza kufikiri Mungu ni mkatili kwa kuruhusu mambo fulani yatokee kwetu. Tunasema, “Mimi ni Mkristo, kwa nini Mungu aruhusu hili litokee kwangu?” Kama baba wa huyu kijana mgonjwa- kadhalika Mungu analo kusudi au fundisho kwa kila jaribu na tatizo ambalo linakuja kwetu. Mbona sasa haturudii, “Ilikuwa vyema kwangu kuwa naliteswa; nipate kujifunza amri zako”(Zaburi 119:71).
Basi kwa nyakati zote na tujifunze kusema, “Ndio, Bwana, mapenzi yako yatimie, hata katikati ya huzuni na majonzi.” Unaweza kuwa na uhakika kwamba pamoja na kila shida Mungu amesha andaa nguvu kwa ajili yako.
“Usiogope mambo yatakayo kupata; tazama, huyo ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima”(Ufunuo 2:10).
Farajika na maneno ya nyimbo hizi zifuatazo:
Mimi ni wako
Nimekujua
Na umeniambia
Lakini Bwana
nataka kwako
Nizidi kusogea
Bwana vuta, vuta,
Nije nisogee
Sana, kwako Mtini
Bwana vuta, vuta,
Nije Nisogee
Pa damu ya thamani.
Mapenzi yako
Hayapimiki
Ila ng’ambo ya liko
Anasa pia sitazijua
Bila kufika kwako.
Nionapo amani kama shwari
Au nionapo shida;
Kwa hali zote umenijulisha
Ni salama rohoni mwangu.
Salama rohoni,
Ni salama rohoni mwangu
Ingawa Shetani atanitesa
Nitajipa moyo kwani
Kristo ameona unyonge wangu
Amekufa kwa roho yangu.