Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembaba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache. Mathayo 7:13-14
Umeshikilia ramani ya maisha. Maisha yetu ni safari. Hapa duniani tunapitia tu. Mungu anapoifikisha safari yako mwisho wake, ni hatima gani inakusubiria katika umilele? Unaona katika maandiko kwamba kuna njia mbili tu. Njia hizi mbili zaelekea katika hatima mbili tofauti. Mungu anakupenda na anakuwazia mema. Anataka uwe naye mbinguni, lakini anakuachia kufanya uchaguzi. Sasa, hebu tuchunguze ramani hii ili tufanye uamuzi sahihi.
Njia Panda Ya Maamuzi
Umati mkubwa, umati mkubwa katika bonde la uamuzi! Kwa kuwa siku ya Bwana ni karibu katika bonde la uamuzi. Yoeli 3:14 NENO
Katika makutano ya barabara, kuna bango limeandikwa, “CHAGUA.” Kuna watu wengi wamesimama katika njia panda ya kufanyia maamuzi. Wanajaribu kuamua njia ipi ya kufuata. Hatima ni Mbinguni au Jehanamu. Uamuzi huu si rahisi kwa sababu njia ielekeayo mbinguni ni nyembamba na ya mwinuko. Jehanamu ni hatima ya kutisha, lakini njia hii ni rahisi kusafiri na ya raha kwa mwili. Yeremia 6:16 inasema, “Bwana asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, I wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu.”
Njia Pana
Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakinimwisho wake ninjiazamauti. Mithali 14:12
Njia hii inaanza ikiwa nzuri sana ikiwa na lango pana na njia pana. Lango hili pana linamaanisha hakuna vigezo – anasa yeyote unayoipenda inaweza kupita. Njia ielekeayo jehanamu imejaa na watafutao kujiridhisha. Kuna ahadinyingitupuzakufahamikanakupatamali, umaarufunakupendwa. Pombe inakufanya usahau majukumu na mahangaiko ya siku yako. Muziki wa sauti kubwa na viburudisho vinakusaidia kusahau mashakanahofuzako.
Lakini unapoendelea katika njia hii wakati mwingine utaingiliwa na wasiwasi. Utaona kila mmoja amebeba mzigo mzito. Mizigo hii ni dhambi ambazo watu wametenda: kusema uongo, kuruhusu mawazo au matendo ya tamaa, kuiba, hasira, au chuki. Kila dhambi inayotendwa inaongezea uzito juu ya mzigo. Hamu ya anasa haiwezi kutoshelezwa; bali inamzamisha mwenye nayo zaidi na zaidi kwenye dhambi. Ingawaje unazungukwa na marafiki wengi, wasafirio njia hii mara nyingi wanazozana na kugombana. Unapowasikiliza unasikia vilio vyao vya kukosa mwelekeo na kuumia moyoni. Wanashangaa kugundua kwamba badala ya kupata uhuru, wameshikiliwa kwa nguvu na minyororo ya dhambi na hawawezi kukwepa! Ni mtego uliotengenezwa na Shetani kwa ajili ya kuharibu nafsi za wanadamu. Njia hii inaongoza kuelekea jehanamu – moto wa milele ambao hautaweza kuzimwa.
Chunguza tena ramani. Kuna matumaini kwa mwenye dhambi. Je, unaona watu wachache waliogeuka na wanarudi kutoka njia hiyo? Watu hawa wamechoshwa sana na maisha yao ya dhambi na wameamua kugeuka, wakiwaacha rafiki na ndugu zao nyuma. Wanaacha vichocheo na anasa za dhambi. Wamedhamiria kukiri makosa yao kabla ya kufika jehanamu. Wameamua kuchagua njia nyembamba.
Ngazi Ya Mkato
Yesu aliwaambia, Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni mnyang’anyi. Yohana 10:1
Kwa bahati mbaya, wengine hujaribu kukwepa kuangamia kwa kutumia nguvu zao wenyewe. Je, unaiona ngazi inayotoka kwa njia hii ya kutisha? Ngazi hii ni njia ya mkato yaShetanikuelekeawokovu, lakininiuongo…..haifiki. Ameutengenezamkatohuuilikudanganyawa tuwaaminikwamba wanaweza kuokolewa bila kupitia njia nyembamba. Njiahiiyamkatohutumiwanawatuwanaojaribusanakuokolewakwabidiizao wenyewe bila kutubu. Labda unafikiri unaokolewa kwa sababu umebatizwa kwa maji au umeombewa na mchungaji. Amapengine, unatafutaukombozi kupitia uponyaji wa miujiza ama kuondolewa mapepo. Lakini unapaswa kujua kwamba katiyavituhivihakunakinachowezakukuleteawokovupasipotobanakubadilika. Soma Mathayo 7:21-23. Unafikiri unaweza ukajipatia wokovukwakuachatumatendoyakomabayana kufanya matendo mazuri. Vipikuhusudhambiulizotendatayari? Mungu hatazisahau. Kwa masikitiko, unaweza ukaona watu wanaotumia ngazi, lakini BADO wanabeba mizigo yao. Mudahaufutidhambi. Maombi na miujiza toka kwa mchungaji hayafuti dhambi. Ubatizo wa maji hauwezi kufuta dhambi. Lazima kupitia kwa njia nyembamba!
Mlangowa Kuingia Kwa Mungu
Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin nawaambieni, Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho. Yohana 10:9
Je, unauonamlangomwembambanamsalaba? Huu ni mlango wa toba ya kweli. Kila msafiri apitaye kupitia njia hii amekuja kwa Yesu msalabani. Wasafiri waliochoka husikia Yesu akiita, “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha” (Mathayo 11:28). Yesu, Mwana wa Mungu, alisulubishwa msalabani na kutoa uhai wake kama dhabihu ya dhambi zetu. Mungu alitangaza kwamba adhabu ya dhambi ilikuwa ni kifo (Mwanzo 2:16-17, Ezekieli 18:20). Kifo cha Yesu msalabani kililipa deni la dhambi zetu; alichukua mahali petu ili sisi tusihitajike tena kufa kifo cha milele. Yesu ndiye njia pekee kufikia uzima wa milele, na ndiye awezaye kuiponya nafsi kutoka kwa ugonjwa wa dhambi. Yesu mwenyewe alisema maneno haya: Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi.” (Yohana 14:6)
Unaona jinsi mlango ulivyosonga? Sisi wenyewe tunaweza kupita kwa uhuru na kuokolewa, lakini hakuna nafasi ya dhambi zetu kupita. Lazima tuziache nyuma. Kila kiburi, tabia za kujivuna lazima ziaachwe mlangoni. Kila kitu lazima kisalimishwe kwa Yesu. Yesu anataka tuzitubu dhambi zetu na kuzikiri kwake. Wakati huo huo lazima KUAMINI kwamba damu yake inaweza kutakasa dhambi zetu na kutupatia moyo mpya. Ni kazi tu aliyofanya Yesu inayoweza kuondoa mzigo wetu wa dhambi na kutupatia amani yakwelimioyonimwetu.
Biblia pia inatufundishakuungamadhambizetukwa wale tuliowakosea (Yakobo 5:16). Hii ni ngumu kwa sababu tunaonea aibu dhambi zetu, tunataka kuzifunika, au kumlaumu mtu mwingine. Soma Yohana 3:19-21 na 1Yohana 1:8-9. Tunaweza tu kuwa huru tukijinyenyekeza na kukiri jinsi tulivyo wenye dhambi.
Njia Iliyo Nyembamba
Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; …Na hao waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuninakuuguazitakimbia. Isaya 35:8, 10
Njia inayoongoza kwenda msalabani na kupitia mlangomwembambayaelekeaMbinguninafurahaya milele. Na ikiwa tutakumbuka hili, itatupa moyo na ujasiri wa kuvumilia magumunamajaribuyoyotetunayokutananayo. Njia hii ni nyembambanayenyemwinuko; nimaishayakujikana nafsi. Kusafiri njia hii kunaweza kukulazimu kuwaacha rafiki au ndugu zako. Lakini kuna furaha na amani ndani ya moyo wako kwa sababu Mungu amekusamehe na kukuondolea mzigo wako wa dhambi. Wale waliopitia njia nyembamba wamepata uhuru wa kweli kupitia kwa Kristo. (2Wakorintho 5:17)
Biblia ni ramani ya wasafiri wa njia hii. Tunahitajika kusoma Neno la Mungu kila siku ili tupate maelekezo. Ni mwangaza wa njia na hutakasa maisha yetu. Pia tumepewa zawadi ya Roho Mtakatifu. Yeye hutuliza mioyo yetu na hutuongoza kwa upole kwa njia nyembamba. Yeye hutusaidia kuzaa tunda la upendo, furaha, amani, uvumilivu, na wema. Tunaweza kuishi kwa maelewano na wenzetu na hata kupenda adui zetu. Tukimfuata na kumtii Roho Mtakatifu pamoja na Biblia, tunahakikishiwa kufika mbinguni salama. Wakati mwingine tunafanya makosa, lakini tukijinyenyekesha na kukiri dhambizetu, Munguatatusamehe.
Njia inapokuwa ngumu, wasafiriwenginehukatishwatamaanakugeuka. Inawezekana wameacha kusoma Biblia na kuomba. Wamepoteza uhusiano wao na Mungu. Soma Luka 14:28-30. Wengine wanaanguka tena katika dhambi zao za kale na kuteleza kutoka njia nyembamba. Ingawa sisi ni Wakristo, bado tunaishi katika miili yenye asili ya dhambi. Ni lazima kuzinyima nafsi zetu vinginevyo tutakuwa nje ya neema ya Mungu. “Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka” Mathayo 10:22
Mwaliko
Dhambi ilizuia ushirika kati ya Mungu na mwanadamu, lakini dhabihu ya Yesu inaweza kuturejeshea amani na kuunga palipovunjika. Mpokee kama Mwokozi wako! Yesu anaweza kukuweka huru kweli kweli! Tubu dhambi zako, salimisha maisha yako kwa Mungu, na wewe pia unaweza kupita njia ya kuelekea mbinguni. Hofu na kutahayarishwa kumepita. Kiu ya dhambi isiyoisha sasa imepita. Badala yake moyo wako uko kwa pumziko na amani. Kuna kutiwamoyo na nguvu ya kutembea njia nyembamba, njia ya kuelekea mbinguni.
Kuna njia mbili tu – Upo katika njia ipi?