Je, ni kwa “njia ya Yesu Kristo”? Au ni kwa “njia ya kimwili”? Njia ya Yesu Kristo ni njia nyembamba. Inaongoza kwenda Mbinguni. Huko Mbinguni hakutakuwa na huzuni wala maumivu, bali furaha na faraja pamoja na Yesu na malaika watakatifu.
Njia ya kimwili ni njia pana. Inatuelekeza kwenye maangamizi, yaani Jehanamu, mahali ambapo kutakuwa na maumivu, maombolezo, na kusaga meno.
Ili kuenenda katika njia ya Yesu Kristo, lazima tuachane na njia ya kimwili. Yesu alisema, “Mtu yeyote akitaka kuwa mfuasi wangu, lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate.” (Mathayo 16:24). Je, kujikana nafsi kunamaanisha nini?
Maana ya kujikana nafsi ni kujizuia katika kutenda uovu au mambo yaliyo na madhara. Tunakataa kutenda mambo yenye tamaa ya kimwili-- ambayo miili yetu kiasili hutamani kuyafanya—mambo ambayo yanatunyima baraka ambazo Baba yetu wa Mbinguni angependa kutolea kwetu. Mtume Paulo ameandika katika Wagalatia 5:19-21, “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.” Leo dunia imechangamana na mambo mengi maovu kama majivuno, kutafuta umaarufu wa kidunia, kusema uongo, tamaa ya kupata mali kwa namna yoyote ile, kutoa talaka na kuachana kwenye ndoa, kuvuta sigara, na kujiingiza katika makundi ya kisiri---tukiweza kutaja machache. Haya yako kinyume na mapenzi ya Mungu, na yataisha pamoja na dunia. Ili tuweze kuwa washindi dhidi ya maovu haya, hatuna budi kusali kwa bidii kumwomba Bwana wetu Yesu Kristo kila siku ili Yeye aweze kutuonyesha ubovu wa tabia hizi na maovu yake. Tunapaswa kumwomba Yeye atupe nguvu ya kutuwezesha tusitende mambo haya.
Ninyi mlio na majina ya kikristo kama Paulo, Maria, Isaka, Yohana, Debora, Gabriel, ama ninyi ambao mmezaliwa katika familia za kikristo na kudhani kwamba hilo linawafanya kuwa wakristo, ama ninyi ambao huenda mmebatizwa miaka mingi iliopita lakini hujaongoka---Tafadhali ieleweke kwenu kwamba hamwezi kuokolewa kutokana na mojawapo wa sababu hizi. Inabidii mjikane na kumfuata katika njia zake yeye.
Tunapaswa kufanya nini wakati tukijikana nafsi zetu?
Jambo la kwanza tunaloweza kufanya ni kusema kwa uthabiti kabisa ni Hapana kwa tamaa zetu za kimwili. Jambo la pili ni kuchukua msalaba wetu na kuanza kutembea katika njia ya Yesu. Kwa baadhi yenu, kuchukua msalaba wako kunaweza kumaanisha kumwacha baba, mama, ndugu, dada, mke wako, mume wako, au rafiki----na kuchukua msimamo upande wa Kristo!
Unapotaka kuwa mkristo ni sharti ujipeleleze wewe mwenyewe na kujua ni wapi ulipopotoka au kutenda dhambi dhidi ya amri zozote zile za Bwana wetu. Ni lazima utubu juu ya uovu wowote ambao umekosea kwayo.
Usife moyo. Yesu atakusamehe iwapo utamjia kwa moyo wako wote. Yeye anasema: “Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mzigo, nami nitawapumzisha.” (Mathayo 11:28). Yeye anataka kukuokoa. Alijikana nafsi yake na akafa msalabani kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote kusudi yeyote atakayekuja kwake aweze kuokolewa.
Kumbuka kwamba kila moja wetu, mkubwa kwa mdogo, atawajibika kwa yale aliyoyatenda au aliyoyasema katika maisha haya (Mathayo 12:36,37).
Tafakari kuhusu ngazi zilizoko katika kurasa za mwisho (kurasa la 4 na 5) na uchague ni ipi ambayo ungependa kutumia. Uwe na uhakika wa kufanya uchaguzi ulio sahihi. Bila shaka---moja ni njia ya Yesu Kristo inayotuongoza kwenda Mbinguni---Utukufu wa milele. Nyingine ni njia ya Shetani---mwisho wake ni Jehanamu.
Njia ya Yesu kwa unyenyekevu huanzia kwa ngazi ya chini na kupanda hadi mbinguni. Njia ya Shetani kwa majivuno huanzia kwa juu na moja kwa moja kuteremka hadi chini kwenye shimo lisilo na mwisho.
Ngazi ya Kwanza:
MILELE MBINGUNI—UTUKUFU!!
Uaminifu hadi mwisho
Kujiepusha na maovu
Ukweli—Ustahimilivu—Wema
Kukomaa katika Maadili ya kikristo
Maisha ya Sala—Utii
Pata Furaha, Amani, Upendo….
Kujikana Nafsi—Chukua msalaba wako
Tubu—Mpokee Yesu kama Mwokozi
Kisikitika dhambi na kuziungama
NJIA YA YESU KRISTO
Njia nyembamba, wachache wataipata
(Mathayo 7:14)
Ngazi ya pili:
NJIA YA MWILI
Njia pana iendayo upotevuni
Wengi huifuata (Mathayo 7:13)
Kukataa njia ya Yesu Kristo
Ubaridi—Uasi—Majivuno
Kufuata tamaa ya mwili
Kuvuta sigara—Kunywa pombe
Kupunja—Wizi—Uongo
Ufisadi—Uzinzi—Talaka
Uasherati—Zaidi ya mke moja
Ibada ya sanamu—Kuabudu miungu
Hamna tumaini kwa Kristo
KUPOTEA KUZIMUNI—MILELE
HUZUNI KUBWA