Injili ya Yohana 10:1-18
Je, umewahi kumsikia mtu akiita jina lako lakini hukufahamu sauti yake ilikuwa ikitokea wapi? Au, hukuweza kusikia sauti kwa maana kulikuwa na kilele nyingi pande zote?
SIKILIZA………sauti inakuita. Wewe!
Wewe ni nani? Jina lako ni nani? Ulitoka wapi? Unakwenda wapi?
Unajua jina la kijiji chako. Inawezekana hujawahi kwenda mahali pengine po pote. Lakini wewe wafahamu kwamba kijiji chako ni sehumu ya nchi kubwa, na nchi zote ni sehemu za ulimwengu mkubwa.
Uumbaji
Ilikuwa ni karibu miaka 6,000 iliyopita wakati ulimwengu ulipoumbwa. Uliumbwa na Mungu. Mungu anacho kitabu kiitwacho Biblia, ambacho kinaelezea jinsi alivyoumba ulimwengu na jinsi alivyowaumba mwanamume na mwanamke wa kwanza. Mungu alimwumba mwanadamu katika mfano wake.
Tangu wakati huo watoto wamezaliwa. Tangu wakati huo watu wamekufa. Maelfu na maelfu wamezaliwa na wamekufa.
Ulizaliwa kutokana na baba na mama yako. Lakini ukweli ni kwamba Mungu ndiye aliyekuumba. Aliumba vitu vyote. Je, umewahi kufikiria jinsi Mungu alivyoumba kila kitu kwa njia ya ajabu na jinsi alivyokuumba wewe?
Wazazi wako walikupa jina. Mungu anajua jina lako. Anajua jina la kila mmoja hata liwe katika lugha gani. Anajua kila kitu.
Kwa sababu Mungu alituumba, anajua yote juu yetu. Anatupenda kwa sababu sisi ni watu wake. Yeye ni Baba yetu aliyepo mbinguni, na anatushughulikia zaidi kuliko baba na mama zetu wanavyofanya.
Mungu
Mungu amekuwepo siku zote, naye anaishi milele. Hivyo basi, alipopulizia pumzi yake ndani mwetu, pumzi hiyo ilitufanya tuweze na sisi kuishi milele daima. Lakini sio kwa miili yetu ya nje (kwa kuwa itakufa), bali roho iliyo ndani mwetu inaishi milele. Je, unamjua Mungu? Huenda unauliza, “Mungu ni nani? Yuko wapi?”
Je, unataka kwa kweli kujua? Ndiyo, ndani mwako unataka ujue.
Hujawahi kumwona Mungu, si ndiyo? Lakini haina maana kwamba yeye hayuko.
Kuna Mungu mmoja tu. Hakuna nafasi kwa mwingine ye yote yule, kwa sababu yeye ambaye ni Mungu kweli kweli anajaza mbinguni na duniani. Yeye yupo mahali pote kwa wakati wote.
Maskani pa Mungu ni mbinguni, mahali pazuri mno hapo juu, lakini pia anaishi mioyoni mwa watu wale wanaoitii sauti yake.
Je, kwa jinsi gani nitaweza kumfahamu Mungu? Je, hili ndilo swali unalojiuliza? Mungu anao mpango wake mzuri wa kutuonyesha ni kwa jinsi gani tungeweza kumfahamu vizuri.
Mungu alimtuma mwana wake wa pekee, Yesu Kristo, kuja hapa duniani kutoka mbinguni ili awaonyeshe wanadamu kwamba yeye ni nani, na jinsi alivyo. Mungu na Yesu kwa pamoja ni kitu kimoja.
Kwa muujiza, Mwana wa Mungu alizaliwa kama mtoto mchanga na alikua hadi akawa mtu mzima. Kisha kwa miaka mitatu, Yesu aliwahubiria watu kuhusu upendo wa Mungu, baba yake. Akawaambia kwamba Baba ni Mtakatifu, na hawezi kuvumilia dhambi.
Ndipo Mungu alitutayarishia njia ili tupate kuokolewa kutoka katika dhambi zetu. Alimruhusu mwanawe Yesu kusulubiwa msalabani kwa mikono ya watu waovu. Aliutoa uhai wake kuonyesha upendo wake ulio mkuu!
Alikuwa ni dhabihu iliyolipia deni ya dhambi zote za ulimwengu mzima-- kwa kila dhambi ulishaitenda, kwa kila dhambi iliyotendwa na kijana, au msichana, au mwanamume, au mwanamke.
Je, Yesu alibakia msalabani? Je, Yesu alibakia kaburini? Hapana, baada ya siku tatu akafufuka kwa ushindi. Ndipo akarudi mbinguni, na anasubiri Mungu atakaposema kwamba dunia imefikilia mwisho wake. Ndipo atakuwa hakimu mwenye haki kwa watu wote.
Je, unayo Injili ya Yohana? Soma sura ya 10. Yohana ameandika yale ambayo Yesu aliwaambia watu. Yale aliyoyasema bado yapo kwa ajili yetu hadi leo. Yesu alisema kwamba yeye ni mchungaji mwema na akatoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. Sisi ndio kondoo. Wale walio kondoo wake wanafahamu sauti yake. Naye huwaita kwa majina yao. Aliye mgeni kwao hawatamfuata.
Sauti ya Mwovu
Ni nani huyo aliye mgeni, huyo ambaye sisi tungemkimbia tungemwona? Aha, kumbe ni mwizi. Ni yule asiyewajali kabisa kondoo. Yeye ni mwongo. Hamna ukweli ndani mwake. Yeye ni Shetani. Ni adui yetu, Shetani.
La kwanza, ni kwamba yeye ni adui wa Mungu. Huko kipindi cha kwanza, aliwahi kuwa malaika mwema akiwa na Mungu huko mbinguni. Mwishowe akaja kuwa na kiburi na kujiinua dhidi ya Mungu. Alipigana dhidi ya Mungu na malaika wengi wakaungana naye. Mungu alishinda kwa sababu anazo nguvu zote. Hatimaye akamtupa Shetani pamoja na wafuasi wake wote kutoka mbinguni. Shetani amemchukia Mungu kwa kitendo hiki.
Kwa sababu hawezi tena kumkaribia Mungu kamwe, anamwaga hasira yake juu ya viumbe vya Mungu, ambavyo ni watu wa ulimwengu. Kwa sababu alitenda dhambi, anajaribu kumshawishi kila mmoja atende dhambi. Dhambi haitaingia mbinguni tena kamwe.
Pana mahali pengine, ambapo Mungu amemwandilia Shetani na malaika zake. Ni Jehanamu. Jehanamu ni mahali pa mateso. Ni moto uwakao ambao hautazimika kamwe. Ni mahali ambapo Shetani na wafuasi wake wataadhibiwa milele. Ni mahali pa kutisha ambapo Mungu atapaswa kututupa ikiwa tumechagua kuisikiliza sauti ya Shetani.
Shetani hapendi sisi tufikirie jehanamu. Hapendi sisi tumkumbuke Mungu. Hiyo ndiyo sababu anajaribu kuondoa usikivu wetu kutoka kwa Mungu. Shetani anajaribu kutufanya tuje kuisikiliza sauti yake tu.
Je, ndani mwako, umewahi kuisikia hio sauti nyingine, sauti ya aliye mwovu?
Mara nyingine, anatudanganya akituahidi kwamba anayo mambo mengine mazuri ya kutupa.
Mara nyingine, anatufanya tuwaze, “Mimi ninao umuhimu kuliko wengine.” “Mimi kwanza, nitapata inavyotarajiwa.” “Ni lazima nipiganie haki zangu.” “Ni sawasawa nikiiba maadamu nisije nikakamatwa.” “Kila mtu anasema uongo, hivyo hata na mimi pia.” “Mawazo machafu siyo mabaya sana, maana hakuna ajuaye yale ninayoyawaza.” “Maneno machafu yanifaa kwa kufurahisha wenzangu.”
Na kwa nyakati zingine unaweza kukatishwa tamaa hadi kujaribiwa ujifikirie kwamba “Mimi sifai, kwa nini niendelee kuishi?”
Haya yote ni sauti itokayo kwa Ibilisi. Yeye ni mwongo. Hiyo ndiyo sababu anajaribu kutufanya tuwe waongo pia. Yeye ni mnyang’anyi, na hiyo ndiyo sababu anatushauri tuwe wanyang’anyi pia. Yeye ni muuaji na hiyo ndiyo sababu anajitahidi kutufanya tuwachukie wengine pia.
Unapoisikiliza sauti kama hiyo, je, inakufanya ujisikiaje? Je, inakufanya uhisi vizuri ndani mwako? La, hasha, inakufanya uhuzunike. Inakufanya utafute pa kujificha. Hivyo ndivyo ilivyo kwa Shetani. Anapenda kufanya kazi yake gizani.
Sauti ya Mchungaji Mwema
Je, unamfahamu Yesu ambaye ni Mchungaji mwema? Je, ungependa kuwa kondoo wake? Ungependa kutambua sauti yake?
Haya basi, unaweza. Lakini jambo la kwanza ni lazima usisikilize hiyo sauti nyingine kwa vyo vyote vile.
Hivyo basi, unapokuwa umetulia, utasikia sauti la utulivu ya Yesu ikikuita ili utoe maisha yako yote kwake. Utamsikia yeye akikwambia kuwa ujutie dhambi zako zote na kuzitubia.
Huenda pia, wakati mwingine, ulikuwa bado umetulia, ulikuwa ukitafakari, “Je, nifanye nini pamoja na matatizo yangu haya yote na mizigo hii?” “Heri ningekuwa mtu mwema.” “Laiti ningekuwapo mahali ambapo nisingeweza kupatwa na njaa wala ugonjwa tena.” “Ni jambo gani litakuwa linanisubiri iwapo nikifariki?”
Huenda pia ukawa una mawazo mengi zaidi. Hiyo ni sauti ya Yesu inayokuita.
Je, kuna wakati mwingine unajisikia umehuzunika bila ya kutambua ni kwa nini? Au unajisikia mpweke wakati ambapo hata ukiwa na watu? Inawezekana ikawa ni kwa sababu unao upweke wa kumkosa Mungu, huyo aliyekuumba na anayekupenda. Yeye ndiye Mchungaji anayekuita. Anamtamani yule kondoo wake aliyepotea. Anakuita na kuita, akikutafuta kwa juhudi.
Unaposikia sauti ya Mchungaji mwema, ebu umwitikie. Mwambie kwamba unazihuzunikia dhambi zako. Mwambie kwa uaminifu jinsi unavyojisikia, na umwombe akuokoe wewe. Hiyo ni kwa njia ya maombi.
Je, umewahi kumwomba Mungu ambaye yuko mbinguni? Fanya hivyo sasa. Atakusikia na kukuelewa. Atakupa amani unayoitamania.
Je, ungependa kuwa kondoo wake na kutambua sauti yake? Anataka awe rafiki yako. Atakuondolea mzigo wa dhambi zako. Utajisikia mwenye furaha ndani mwako. Utakuwa mwenye upendo na huruma sawa na jinsi alivyo yeye. Atakusaidia kuzishinda hofu zako.
Hata kama wengine watakusumbua kutokana na imani yako, tambua vizuri kwamba Yesu atakuwa mwangalizi wako. Hata kama yule mwovu atakujaribu tena ni lazima umtegemee Yesu kukusaidia ili ushinde.
Unapokuwa salama katika mikono wa Mchungaji mwenye upendo, tambua kwamba utakapofikia mwisho wa safari yako, atakulaki uishi naye katika mji wake wa ajabu ambako kuna furaha na amani tele.