Vipeperushi
Hapo mwanzo, Mungu aliumba mbingu na nchi. Aliumba jua, mwezi, na nyota, na pia mimea na wanyama. Siku ya sita, aliumba mtu kwa mfano wake na akampulizia puani pumzi ya uhai. Mtu huyu wa kwanza alikuwa Adamu, na jina la mkewe aliitwa Eva. Mungu aliwapa makao ya kuishi katika bustani nzuri ya Edeni. Mungu aliwapenda Adamu na Eva, nao walimpenda Mungu. Mungu alimwagiza Adamu kuitunza bustani. Mungu aliwaambia kua wanaweza kula chochote watakacho isipokuwa kwa mti wa ujuzi wa mema na mabaya, na ya kuwa watakufa kama hawatatii.
Imeandikwa na John Reynolds Mojawapo ya mifano iliyohai na ya kuvutia kabisa ya kurudishiwa uhai wa mtu aliyekwisha kufa ambao nimewahi kuufahamu ulikuwa ni ule wa George Lennox, mwizi stadi wa farasi kutoka Jimbo la Jefferson (Marekani). Alikuwa akitumikia kifungo chake cha pili. Jimbo la Sedwick lilimpeleka gerezani kwa mara ya kwanza kwa kosa hilo hilo – wizi wa farasi.
Kama inavyotumika katika kitabu hiki, “moyo wa binadamu” humaanisha kikalio cha mapenzi yetu, au “wewe halisi”. Mungu hamtazami binadamu kwa nje, bali hutazama ndani ya moyo wake. Hakuna kilichofichika kwa Mungu.
Je, wewe ni mwenye furaha? Au hofu na hatia huondoa furaha yako yote? Je, ungetamani kuondoa hatia yako, lakini hujui kwa njia gani? Huenda unajiuliza, “Je, nitawahi kuwa mwenye furaha tena?” Ninayo habari njema kwa ajili yako. Kuna Mmoja awezaye kukusaidia, kusamehe dhambi zako, na kukupa furaha ya daima. Jina lake ni Yesu. Ngoja nikuambie habari zake. Mungu ndiye mwenyewe aliyeumba ulimwengu na vitu vyote vilivyomo. Alikuumba wewe na mimi.
Lengo la Biblia Takatifu silo kuangalia hasa Shetani na kazi zake. Japokuwa tunapata mengi kwenye Biblia yanayofunua tabia zake na kazi zake. Wakati fulani Shetani alikuwa malaika, lakini aligeuka kinyume cha Mungu, Muumba wake, na akatamani kuwa kama Mungu. Matendo ya ufalme wa giza wa Shetani siyo mageni. Yanaonyesha dhahiri jitihada za Shetani kwa miaka kupingana na Ufalme wa Mungu. Anatoa mbadala wa kile ambacho Mungu anatimiliza kwa kupitia nguvu za Roho Mtakatifu.
Yesu Rafiki Yako Ninaye rafiki. Yeye ndiye rafiki bora ambaye nimewahi kujua. Yeye ni mwema sana na mkweli ambaye na wewe pia ningependa umfahamu. Jina lake ni Yesu. Cha kustajaabisha ni kwamba na yeye angependa awe rafiki yako. Ngoja nikuambie habari zake. Tunasoma hadithi hii katika Biblia. Biblia ni kweli. Ni neno la Mungu. Mungu ndiye aliyeumba ulimwengu na vitu vyote vilivyomo. Yeye ni Bwana wa Mbinguni na dunia. Anatoa uzima na pumzi kwa viumbe vyote.
Injili ya Yohana 10:1-18 Je, umewahi kumsikia mtu akiita jina lako lakini hukufahamu sauti yake ilikuwa ikitokea wapi? Au, hukuweza kusikia sauti kwa maana kulikuwa na kilele nyingi pande zote? SIKILIZA………sauti inakuita. Wewe! Wewe ni nani? Jina lako ni nani? Ulitoka wapi? Unakwenda wapi? Unajua jina la kijiji chako. Inawezekana hujawahi kwenda mahali pengine po pote. Lakini wewe wafahamu kwamba kijiji chako ni sehumu ya nchi kubwa, na nchi zote ni sehemu za ulimwengu mkubwa.
Tunaishi katika ulimwengu ambamo kila mmoja hupenda kutoa udhuru. Karibu kwa kila jambo linalogusa moyo wako hutaki kukubali au kuukabili ukweli jinsi ulivyo, kwa hiyo unatafuta njia ya kujitetea, ukidhania kwamba utetezi wako utakuweka huru. Je, unafikiri udhuru zako zitakuweka huru mbele za Mungu? Je, kuokolewa kunao udhuru? Visingizio ulivyo navyo kwa uhakika havitakuweka huru. Adamu na Hawa walipotenda dhambi, kila mmoja alijaribu kumtupia mwenzake lawama ya dhambi iliyotendeka, wakidhania kwamba Mungu angeachilia dhambi yao kwani wametoa sababu ni kwa nini waliingia dhambini. Lakini bado twasoma katika Biblia kwamba Mungu aliendelea kuwaadhibu tu. Mungu hazikubali udhuru zetu, hata zipangiwe kwa hila ya namna gani, au hata ukijifanya uonekane kuwa msafi kiasi gani. (Mwanzo 3:9-19; Wagalatia 6:7-8).
Bwana Yesu alikuja ulimwenguni kuwaokoa wanadamu kutoka kwa dhambi zao. “Bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa akawa ana mfano wa wanadamu” (Wafilipi 2:7). Alikufa kwa ajili ya dhambi za watu wote ulimwenguni, alizikwa na akafufuka tena (1Wakorintho 15:4), kisha akapaa kwenda mbinguni tena (Matendo 1:9). Mitume walimwona na pia waumini zaidi ya mia tano, baada ya kufufuka. Baada ya kupaa kwenda mbinguni, malaika wawili waliwaambia mitume kwamba kurudi kwake kutafanana na kupaa kwake. Ni Mungu tu ndiye anayefahamu ni lini Bwana atarudi. Huenda itakuwa ni jioni au usiku wa manane, au wakati wa asubuhi au alasiri. (Marko 13:35) “Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja” (Mathayo 24:44).
Kabla ya muda haujakuwepo Mungu alikuwepo. Aliumba dunia na kila kitu kilichomo. Katika upendo wake, Mungu akaumba mwanadamu kwa sura yake mwenyewe akawaweka kwenye bustani nzuri. Wanadamu hawakutii maelekezo ya Mungu. Kutokutii huku kulikuwa ni dhambi iliyowatenganisha mbali na Mungu. Aliwaambia kwamba wanapaswa kutoa dhabihu za wanyama wadogo wasio na madoa yoyote kwa ajili ya dhambi zao. Dhabihu hizi hazikulipia dhambi zao bali zilielekeza dhabihu ya mwisho ambayo Mungu angetoa. Siku moja Mungu angetuma mwanawe Yesu duniani awe dhabihu ya mwisho.